Rekodi Mauzo kwa Haraka
Andika mauzo ya leo kwa sekunde chache — hata kama bidhaa haipo kwenye orodha bado (unaweza kuandika tu).
Indeii inakusaidia kuanza na jambo moja muhimu: rekodi mauzo. Kisha, unapohitaji kuona biashara yako vizuri zaidi, fungua ripoti kamili (mwenendo, faida, stock, na zaidi).
🇹🇿 Imetengenezwa kwa biashara za Tanzania — maduka, supermarket, mafundi, salon, na wazalishaji.
Imetumika na biashara nyingi — na inaendelea kukua.
Andika mauzo ya leo kwa sekunde chache — hata kama bidhaa haipo kwenye orodha bado (unaweza kuandika tu).
Fuatilia stock na upate taarifa bidhaa zinapokaribia kuisha. Inakusaidia kujipanga mapema.
Kwa maduka yenye bidhaa nyingi: scan barcode, ongeza cart, chagua njia ya malipo, na toa chenji haraka.
Kwa wazalishaji (keki, mafuta, juice n.k.): weka malighafi + vipimo vya “recipe”, Indeii itajua gharama halisi ya bidhaa.
Ukitaka kuelewa biashara yako zaidi, fungua ripoti kamili (mwenendo, faida, bidhaa zinazoongoza, na zaidi).
Ujumbe wa kusaidia tabia ya “rekodi kila siku” na kumbusho la kufunga siku (bila kukukwaza).
Rekodi mauzo, matumizi na manunuzi bila kuzuiwa. Unalipia pale unapohitaji ripoti kamili.
Fungua ripoti kamili kwa mwezi
Bora kwa biashara zinazoendelea
Kwa biashara inayokua
Bei bora kwa mwaka mzima
Unahitaji mpango wa POS (barcode) au uzalishaji (recipe costing)? Wasiliana nasi — tunakuweka sawa.
Ndiyo. Unaweza kurekodi mauzo, matumizi na manunuzi bila kuzuiwa. Ukihitaji ripoti kamili (faida, mwenendo, n.k.) ndipo unafungua kwa kulipia.
Indeii ina POS (hasa kwa tablet/desktop) na barcode scanning kwa maduka yenye bidhaa nyingi. Lakini kazi yake kubwa ni kukusaidia uione biashara yako kupitia ripoti na uelewa.
Ndiyo. Unaweza kuingiza kwa Excel/CSV, au utumie “quick add” uki-scan barcode bidhaa ambayo haipo.
Unaweka malighafi + gharama zake, kisha unaweka “recipe” (vipimo). Ukizalisha, Indeii inajua gharama halisi ya bidhaa na inapunguza stock ya malighafi moja kwa moja.
Ni rahisi. Kwanza rekodi mauzo. Ukihitaji uelewa zaidi, fungua ripoti kamili — na uone biashara yako vizuri.